Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini hujambo na unaendelea vizuri kuifanya dunia kuwa sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu. Rafiki, mimi na wewe ndio tunafanya dunia kuwa sehemu salama au silama kuishi kwa kila mmoja wetu. Hivyo basi, yatupasa tuwe sehemu ya mabadiliko tunayotaka kuyaona katika hii dunia na siyo kuendelea kulalamika. Mpemdwa msomaji napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja makala nzuri niliyokuandalia siku hii ya leo.
Leo tutajifunza kwa pamoja rafiki yangu kiungo hatari sana cha mwanadamu kinachoongoza kuuwa katika zama hizi au karni hii ya ishirini na moja (21). Kumekuwa na watu wengi katika zama hizi wanaoua kwa kutumia kiungo kidogo sana katika mwili ambacho ni ulimi. Ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili wa binadmau lakini kinaleta athari kubwa sana katika maisha ya watu. Tumekuwa na wauwaji wengi katika jamii zetu wanaoua watu kwa kutumia ulimi. Ulimi huu unafanya maisha ya watu kuwa machungu kwa kuchomea makombora ya umbea, majungu,unafiki, wivu na chuki ambayo chuki huwa inazaa mauti katika jamii zetu. Ulimi huu unafanya familia zinatengana,watoto wanaoishi mazingira hatarishi wanaongezeka kwa sababu ya madhara ya ulimi. Ulimi unaleta madhara makubwa sana katika maisha yetu.
SOMA; Ifahamu Nguvu Ya Kusema Hapana Katika Maisha Yako
Migogoro mingi inayotokea kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu chanzo chake kinakuwa ni kutumia ulimi vibaya. Mtu anaongea tu bila kufikiri kwa kina je haya maneno ninayoongea yataleta athari gani baadae. Kauli mbovu zinazochochea uchochezi katika jamii zetu zinasababishwa na hiki kiungo kidogo sana cha binadamu ambacho ni ulimi. Watu wanatishiana maisha kwa kutumia kiungo hiki cha ulimi na kiungo hiki kinatumika kuvunja mahusiano ya watu na pia ndio kiungo pekee kinachoweza kurudisha uhusiano uliovunjika. Kiungo hiki kinakuwa kina hukumu watu bila hata ya kuujua ukweli na kuwapa watu nafasi ya kujieleza kwa mambo waliofanya. Kiungo hiki kama ukikitumia vizuri utajenga jamii iliyo bora sana na kama ukitumia vibaya kupandikiza chuki basi utajenga jamii iliyo mbovu sana.
SOMA TENA; Huu Ndio Umuhimu Wa Kujenga Mahusaino Bora Katika Maisha Yetu
Hatua ya kuchukua; tumia ulimi wako vizuri. Fikiri kabla ya kuongea na kujiuliza maswali je hiki nitakachoongea kitaleta athari gani katika jamii? Fikiri kabla ya kunena, fikiri kabla ya kutenda. Tumia ulimi wako vizuri kurudisha uhusiano uliovunjika na kuifanya dunia kuwa sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu.
Mwisho, katika somo letu la leo tumealikwa sisi sote kuchunga ndimi zetu kwani ndimi zetu zinaleta athari chanya na hasi katika jamii yetu. Ni kiungo kidogo sana katika mwili wa binadamu lakini kinaleta athari kubwa kwa jamii yetu. Tuchunge ndimi zetu na tufikiri kabla ya kunena. Tutumie ndimi zetu kujenga mazuri katika jamii zetu na siyo maovu.
Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.
[mailerlite_form form_id=1]
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com