Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifahamu Nguvu Ya Kusema Hapana Katika Maisha Yako

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu hujambo na unaendelea vizuri kuhakikisha unapambana na hatimaye kupata kile kilicho bora. Tumia nafasi yako uliyonayo sehemu uliyopo kuleta mabadiliko ya jamii inayokuzunguka. Kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona katika maisha yako ndiyo njia bora na ya uhakika ya kufanikiwa. Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Rafiki, ili uendele kupata makala za ziada zenye mafunzo mbalimbali tafdhali jiunge sasa katika mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email yaani email list.  [mailerlite_form form_id=1]

Image result for THE POWER OF SAY NO IN OUR LIFE

Mpenzi msomaji, katika makala yetu ya leo tutajifunza nguvu ya kusema hapana katika maisha yetu. Nakusihi tusafiri pamoja ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja makala nzuri niliyokuandalia leo rafiki yangu. Katika dunia ya sasa unahitaji kusema hapana kwa vitu vingi ili uweze kufanikiwa katika maisha yako. Kuna nguvu kubwa ya kusema hapana katika maisha yako na ikakusaidia kupiga hatua kubwa katika maisha yako. Dunia ya sasa imejaa kelele nyingi sana na usipokuwa makini lazima kelele hizi zitakuchanganya na hatimaye kupotea. Kuna mambo mengi sana hivyo huwezi kufuatilia kila kitu katika hii dunia bali unatakiwa kusema hapana kubwa kwa vitu ambavyo havina msaada katika maisha yako. Kama kuna mambo yanakusumbua katika maisha yako huu ni wakati wa kusema hapana.

MUHIMU SOMA;  Huyu Ndiye Chuma Ulete Anayewatesa Watu Wengi Katika Maswala Ya Kiuchumi

Rafiki, unatakiwa kuanza kusema hapana katika kila idara ya maisha yako ili uweze kufanikiwa. Huwezi kupata ukombozi wowote katika maisha yako kama hujasema hapana kwa kile kitu kinachokuumiza. Sema hapana kwa uvivu, uvivu ni mbaya na hauna nafasi katika jamii yetu unapaswa kuepuka uvivu kwa kusema hapana. Uvivu ndio unazaa utamaduni wa walalamikaji wengi katika jamii yetu. Sema hapana kwa wivu katika maisha yako. Kama uko katika dunia hii ya leo unatakiwa kuondoka katika hisia za wivu kwani wivu ni ujinga ambao hautakufikiasha sehemu yoyote bali utakufanya uishi maisha ya shinda na ya kuteseka.

Sema hapana kwa kupoteza muda katika mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ina faida na athari zake pia na mitandao ya kijamii imekuwa ndio kinara wakupoteza wakati katika zama hizi za taarifa. Kwa mfano, unakuta mtu yuko katika magrupu zaidi ya matano katika simu yake yaani akija tu kuwasha data anakutana jumbe nyingi zisizopungua chini ya mia tano. Sasa kama unataka kuondokana na tatizo hili njia nzuri ni kusema hapana. Unasema huna muda wa kusoma kitabu wakati kwa siku unasoma jumbe nyingi ambayo nguvu hiyo ungekuwa unaiweka katika kusoma vitabu kwa wiki ungekuwa unasoma hata vitabu visivyopungua vitatu. Sema hapana kwa kupoteza muda katika mitandao ya kijamii kila siku na tumia rasilimali hiyo kuboresha maisha yako.

Sema hapana katika kulaumu na kulalamika. Moja ya changamoto ya watu wengi siku hizi ni kulalamika na kulaumu. Unakuta katika ofisi bosi ni mlalamikaji, wafanyakazi ni walalamikaji kuanzia kiongozi wa juu mpaka mlinzi wa getini ni mlalamikaji. Hatuwezi kufika mbali kwa kulalamika tunaweza kufika mbali kwa kusema hapana. Watu wanalaumiana kila mmoja anaona yeye hajakosea ila mwenzake ndiyo amekosea hivyo tabia ya kulaumiana imegeuka kuwa utamaduni wa watu wengi. Usilalamike juu ya serikali na kuweka matumaini yako huko kwani utapoteza muda na kuangushwa kila siku. Aliyekuwa raisi wa awamu ya 40 wa marekani Ronald Reagan aliwahi kusema ‘’serikali ni matatizo na serikali siyo suluhisho la matatizo yetu’’ rafiki kama ulikuwa unategemea serikali ukweli ndio huo.

SOMA KALI NYIGINE;  Hii Ndio Mbinu Bora Ya Kumsaidia Mtu Ambaye Hajui Kwenda Na Muda Kwenye Maisha Yake
Hatua ya kuchukua; sema hapana kwa mambo yanayokupotezea muda, sema hapana kwa mambo yanayokufanya ukose furaha, sema hapana kufuatilia siasa ili ujiepushe na msongo wa mawazo. Acha kuangalia tv na kufauatilia habari, tamthilia,umbea, majungu,mambo yasiyokuhusu nakadhalika. Sema hapana kwenye kila idara inayokwenda vibaya usiruhusu kusema ndio kwani ndio inaruhusu mafuriko ya matatizo kwenye maisha yako.

Kwahiyo, mpenzi msomaji, somo letu la leo limetualika kusema hapana katika mambo ambayo hayana faida chanya katika maisha yetu. Unatakiwa kusema hapana ili uweze kufanya mambo ya msingi na ukiruhusu kusema ndio kwenye kila jambo huwezi kufika kule unakotaka kwenda. Hapana ina nguvu kubwa katika maisha yetu na tuitumie kuleta mabadiliko katika jamii zetu. Kila mtu awe balozi wa kusema hapana na mshirikishe mwenzako maarifa haya mazuri ili aweze naye kujifunza.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

[mailerlite_form form_id=1]

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: