Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini unaendelea vizuri rafiki yangu na hongera kwa kuwa na mwisho wa juma mzuri ambao ni muda mzuri kwako kupangilia wiki yako ya kesho unataka iendeje. Usianze siku bila kuandika malengo ya siku husika na wiki nzima kwa ujumla. Malengo yanatakiwa yaandikwe kwenye daftari na siyo kukaa kichwani. Basi, mpendwa rafiki yangu nikualike tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Tafadhali nakusihi ungana nami katika safari hii ili uweze kujua yale mazuri niliyokuandalia leo. Katika makala yetu ya leo tutaweza kujifunza njia bora ya kuokoa mawazo yetu. Karibu tujifunze kwa pamoja.
Aidha, Kuna aina mbili za fasihi nazo ni fasihi andishi na fasihi simulizi (written literature & oral literature). Fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayowasilishwa kwa njia ya mdomo na fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Sasa mpenzi msomaji katika hali ya kawaida tunakuwa na mawazo mengi katika maisha yetu ambayo kama tusipo ya hifadhi hupotea bila kujua. Ni rahisi kusema kwa mdomo kuwa hapa nimeelewa na mafundisho mazuri niliyopata siwezi kuyasahau hata kidogo. Mwingine anakuwa na mawazo (ideas) nzuri sana lakini anahifadhi akilini yaani kichwani na hatimaye anakuja kusahau. Kichwa cha binadamu kina mambo mengi hatuwezi kuhifadhi kila kitu kichwani hivyo ni muhimu kuwa na njia bora ya kuokoa mawazo yetu.
SOMA; Huu Ndio Ukombozi Wa Akili Unaopaswa Kua Nao Kuanzia Sasa Kwenye Maisha Yako
Huenda ulikuwa unajiuliza ni njia zipi unaweza kuzitumia hatimaye kuokoa mawazo yako? Njia bora ya kuokoa mawazo yako yasipotee bila kujua ni kuandika tu. Chochote unachotaka kufanya au unachofikiria andika mara moja katika daftari ili lisipotee kichwani. Usipate shinda sana ya kuhifadhi kila kitu kichwani wakati kuna njia nzuri mbadala za kuhifadhi mawazo yetu. Huna haja ya kuhifadhi kila kitu kichwani kwani kuhifadhi mawazo kichwani ni sawa na kuweka mshumaa katika upepo muda wowote unazima. Hivyo basi, njia ya kuandika ni njia bora sana ya kuhifadhi kumbukumbu yoyote ile.
Hatua ya kuchukua; nunua daftari na kalamu na andika kila wazo linalokuja katika akili yako.
Pili, tembea na kalamu na daftari sehemu yoyote unayoenda wazo tu likikujia unaandika kwani kwa kufanya hivi utakua unakoa mawazo yako. Kama unatumia simu aina ya smart phone kuna sehemu ya kuandika unayoweza kuhifadhi mawazo yako yasipotee. Pia, katika simu kuna sehemu ya kurekodi hivyo kama umeshindwa kuandika unaweza tu ukaongea na kujirekodi halafu baadae unakuja kuandika.
SOMA; Hili Ndilo Tatizo Linalowasumbua Watu Wengi Kushindwa Kutimiza Ndoto Zao
Mwisho, akili yako ni kiwanda kinachozalisha maarifa hivyo yaokoe mawazo yako kwa kuandika chini ili yaweze kukusaidia. Hivyo njia ya pekee na bora ya kuokoa mawazo yako ni kuandika tu. Somo letu la leo limetualika kuokoa mawazo yetu kwa kuyaandika na siyo kuhifadhi kwa njia ya kichwani. Akili yako ni kiwanda kinachozalisha mawazo ya utajiri.
[mailerlite_form form_id=1]
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com
Leave a comment