Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa wa Kessy Deo, natumaini uko salama rafiki yangu na unaendelea vizuri kuboresha maisha yako lakini pia kuwasaidia wengine kwa namna moja au nyingine. Mpendwa rafiki, ungana nami katika makala yetu ya leo tuweze kuanza pamoja hadi tamati ya makala hii.
Kila mtu anahitaji kuwa na maisha mazuri na mengine mengi kulingana na hitaji la mtu alilolichangua kuwa nalo kwenye maisha yake. Wengi huishia kuongea ndoto zao mdomoni hatimaye wanakufa na ndoto zao bila hata kuzifanyia kazi. Tunakua na machaguo mengi katika maisha yetu ambayo hatuyafanyii kazi kwa vitendo kama ingekuwa kila mtu anatumia mawazo yake vizuri na kuyafanyia kazi basi dunia ingekua bora sana na kila mtu angekuwa bora. Tofauti yetu kubwa sisi binadamu iko katika akili tu. Akili yako ni kiwanda kinachozalisha maarifa je unayatumia mawazo yako vema kuboresha idara mbalimbali kwenye maisha yako?
SOMA HAPA; Hili Ndilo Hitaji La Kwanza La Mwanadamu Katika Maisha Yakela-kwanza-la-mwanadamu-katika-maisha-yake
Niliwahi kuhudhuria semina siku moja mahali Fulani katika semina hii mama mmoja alisema kulingana na mapito aliyopitia katika maisha yake lazima siku moja atakuja kuandika kitabu ili na wengine waweze kujifunza juu ya mapito hayo aliyopitia. Akaongezea na kusema akipata muda ataandika kitabu. Sawa mama alikuwa na mawazo mazuri sana na lakini nina imani mpaka leo Yule mama bado hajaandika kitabu na wala hatakuja kuandika kitabu. Kwa sababu gani kwanza, hana uhakika ni lini atakuja kuandika kitabu kwasababu hajasema ataanza lini na wakati wa kuanza ni sasa. Pili, mama alikuwa ni mtu wa makamu umri wake ulikuwa umeenda halafu alisema tatizo kwake ni muda hivyo anasubiri ukamilifu wa muda pengine ndio aandike kitabu na hakuna ukamilifu hapa duniani.
SOMA ZAIDI; Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yao
Ndugu msomaji, shabaha yetu leo ni kujua tatizo linalowasumbua watu wengi kushindwa kutimiza ndoto zao. Je tatizo hilo ni nini? Tatizo linalowasumbua watu wengi kushindwa kutimiza ndoto zao ni KUANZA. Hakuna kitu kingine rafiki yangu watu wanakua na mawazo mazuri lakini tatizo ni kuanza kwenye kile anachotaka kufanya. Kwa mfano, mtu anapenda kuacha kuvuta sigara lakini anashindwa kuanza kuacha kuvuta sigara. Mwingine anatamani na yeye maisha yake yabadilike lakini anashindwa kuchukua hatua za kuanza.
SOMA HII; Huu Ndio Uwekezaji Muhimu Unaoweza Kuanza Nao ambao Mtaji Wake Tayari Unao
Kila mtu asikubali kufa na mawazo yake kwa sababu ya kushindwa kuanza leo. Tafadhali wewe anza hivyo hivyo ulivyo na hapo hapo ulipo. Usisubiri mpaka upate ukamilifu ndio uanze kuchukua hatua. Kusubiri ukamilifu ni sawa na kusubiri kuvuta pumzi ya mwisho hapa duniani hujui siku yako ya mwisho kuvuta pumzi hapa duniani ni lini na ni wapi. Usikubali kusumbuliwa na tatizo la kushindwa kuanza rafiki. Kwa mfano, watu wanadharau vidogo walivyonavyo sasa ukweli ni huu kama umeshindwa kufanya kitu kwa kidogo ulichonacho hata ukipata kikubwa hutoweza kufanya kitu utaendelea kuwa mbinafsi zaidi ya ulivyokuwa mwanzo. Kitumie kile ulichonacho sasa kubadili hali uliyo nayo sasa.
SOMA MUHIMU; Ifahamu Falsafa Muhimu Sana Katika Maisha Yako Kutoka Kwa Mwanafalsafa Ralph Waldo Emerson
Hivyo basi, acha kuongea ndoto zako kwa mdomo bali ongelea ndoto zako kwa vitendo kwa kuanza leo. Uhai wa ndoto ni kuanza leo. Usisubiri upewe ruhusa na wakati sahihi ni sasa. Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com
Leave a comment