Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Ishirini (20) Niliyojifunza Katika Kitabu Cha The Leader Who Had No Title

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa Kessy Deo. Natumaini hujambo na unaendelea vizuri.
Karibu Rafiki nikushirikishe mambo muhimu niliyojifunza katika kitabu cha The Leader Who Had No Title.
Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha
The Leader Who Had No Title na Robin Sharma ni kama ifuatavyo;
Utangulizi:
Robin Sharma ni mwandishi mashuhuri duniani aliyejitoa katika kusaidia watu duniani kupitia mafundisho yake anayotoa kwa njia mbalimbali.
Hiki ni kitabu muhimu kitakacho muonesha kila binadamu jinsi gani au namna gani anaweza kuonyesha uongozi katika yote anayofanya na hatimaye kuongeza thamani katika eneo aliopo.
Na karibu tushirikishane mambo haya niliyojifunza.

1. Kama umebarikiwa kuwa na mzazi mpaka sasa basi waheshimu na fanya hivyo kila siku. Wazazi ni zawadi kutoka Mungu hivyo yatupasa kuwaheshimu na kuwapenda kama walivyo.
WApende kama walivyo bila kujali udhaifu wao.
Wazazi ndio njia ya kila mwanadamu kuja hapa duniani. Bila mzazi wewe usingekuwepo. Ondoa tabia ya kuchukia watu bila sababu wapende kama wazazi wako.

2. Kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu ni silaha kubwa katika kutafuta maarifa hapa duniani. Vitabu ni mwongozo wa maisha yetu. Watu wa kubwa siku zote huonekana kuwa na maktaba kubwa.
Hatua; Wajengee watoto desturi ya kusoma vitabu tangu wakiwa wadogo.
Onyesha mfano katika familia yako katika usomaji wa vitabu.
Kuwa motisha na hamasa kwa familia,na jamii iliyokuzunguka katika kuhamasisha usomaji wa vitabu.

3. Ili taasisi iweze kukua kila mmoja lazima ajione yeye ni sehemu ya uongozi kama timu. Bila kujali cheo ulichonacho hapo ulipo unachotakiwa ni kuongoza bila kuwa na cheo. Hakikisha hapo ulipo unapatendea haki onesha uongozi wako na kuwa sehemu ya mabadiliko. Kama hapo ulipo ni pachafu fagia usisubiri uambiwe.

4. Kila mmoja anahitaji aendeleze uvumbuzi au ugunduzi. Kila mmoja anatakiwa kuwahamasisha wafanyakazi wenzake.
Kila mmoja anahitaji kukubali mabadiliko. Kuwajibika juu ya matokeo,kuwa mtu chanya na kujitoa au kujicomit katika ubora wa hali ya juu.

5. Kila kazi ni kazi muhimu. Kila mtu ni mkurugenzi mtendaji wa wajibu wake mwenyewe. Hupaswi kusuburi kupewa cheo ndio uongoze. Kila mtu anaweza kuongoza na kila mtu anayefanya kazi lazima aongoze.
Hivyo kuongoza hakuitaji mpaka uwe mtu mkubwa sana hapana bali kuwa sehemu ya hapo ulipo. Simamia kazi yako unayofanya kwani wewe ndio mkurugenzi wa kazi yako una uwezo wa kufanya iwe bora au hovyo. Heshimu kile unachofanya na fanya kwa uhakika na ufanisi mzuri.

6. Kama ilivyo ada unavyokwenda katika mgahawa ili upate chakula ni lazima ulipie bei ili uweze kupata huduma. Vivyo hivyo katika kazi na maisha yetu kwa ujumla unahitaji ulipe bei ya mafanikio.
Maisha yetu yana gharama na kila kitu kina bei yake.
Siku zote utavuna ulichopanda na utapata kile unachostahili.

7. Pesa ni muhimu sana ili kuishi maisha yako yenye ubora hapa duniani. Pesa huleta uhuru na kupunguza msongo wa mawazo.
Itakuruhusu kupata huduma nzuri unayoipenda.
Hivyo fedha ni muhimu sana katika maisha yetu ya leo.

8. Njia nzuri ya kumsaidia mtu maskini ni wewe kuwa tajiri. Au kwa lugha nyingine kama unataka kuwasaidia watu duni njia ni ya wewe usiwe kama wao. Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake .

9. Kuongoza bila kuwa na cheo ni falsafa inayohitaji kuwa na nidhamu.
Huwezi kuongoza kama wewe mwenyewe huna nidhamu.
Katika kuongoza bila kuwa na cheo inahitaji nidhamu ya kujifunza.
Katika kujifunza kurudia kurudia ndio njia pekee ya kujifunza. Bila kurudia hujifunzi kitu mfano umesoma leo basi husomi tena kwa njia hii huwezi kujifunza kitu.
Kujifunza ni kurudia hakuna mwisho katika kujifunza.

10. Kama kila mmoja akijitoa katika yake na kuipenda kazi yake basi mambo yangekuwa mazuri sana.
Watu wengi wanafanya kazi wasizozipenda ndio maana manung’uniko hayaishi kila siku.
Ufanisi wa kazi utakuja pale mtu anapopenda kazi yake anayofanya.

11. Watu ambao wako vizuri katika kutafuta sababu mara nyingi huwa wanakuwa si watu kutenda sana. Falsafa ya hii ya ongoza bila kuwa na cheo huwa haitaji watu wa sababu. Watu makini waliojitoa ndio wanaweza kuendana au kurandana na falsafa hii nzuri.

12. Bila kuwa na ugunduzi au uvumbuzi hakuna maisha. Dunia inabadilika kila siku kulingana na uvumbuzi wa watu mbalimbali.
Ulianza mfumo wa analojia ambao kwa sasa hauna nafasi tena. Uvumbuzi umefanyika ukaleta matokeo ya digital. Uvumbuzi umeleta matokeo chanya kwa jamii yetu.
Hivyo, maisha ni ugunduzi bila ugunduzi hakuna maisha.

13. Kuahirisha mambo ni aina nyingine ya hofu. Wakati watu wanatumia muda wao vizuri kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wengine wanatumia muda wao vibaya. Wakati wewe umekaa kwenye kochi unaangalia tv mwenzako ameshika kitabu anasoma na kutafuta maarifa.
Hivyo basi,wote tunauwezo wa kufanya mambo tofauti ni uelewa tu na nidhamu ya kusimamia.

14. Unatakiwa uwe na malengo yanayokuongoza katika kazi yako. Unahitaji kuwa na kitu au sababu itakayokusukuma uruke kutoka kitandani asubuhi. Na kuanza kuwasha moto wa kufanya kazi. Huwezi kuamka mapema halafu huna kitu cha kufanya lazima uwe na sababu inayokusukuma kuamka mapema kila siku asubuhi.

15. Kuwa halisi,kuwa mwaminifu,heshimu wengine pia. Dunia ya leo inahitaji uwe halisi,usiwe mtu wa kuigiza ya watu wengine. Kama kiongozi unatakiwa kuwa na msimamo na kuonesha uhalisia wako.

16. Changamoto kubwa ya watu katika kufanya jambo ni kushindwa kukomaa au kung’ang’ania kitu anachofanya mpaka kufanikiwa. Huwezi kuona umuhimu wa kufanya jambo na matokeo kama wewe ni mtu wa kugusa na kuacha kufanya kingine. Hivyo basi,uvumilivu na kung’ang’ania mpaka unafanikiwa ndio njia kuu ya kufikia mafanikio.

17. Tunaishi katika dunia ya mabadiliko. Hivyo mabadiliko yanaleta fursa kwa watu. Tunapata somo kubwa kupitia mabadiliko na tunapaswa kujifunza katika mabadiliko. Kukataa kujifunza kupitia mabadiliko ni kukwepa maendeleo.

18. Maneno yako yanaleta nini kwa watu?
Maneno yako yaonyeshe uwezekano kwa watu.
Maneno yako yalete furaha kwa watu kwa watu na kujihisi wenye amani. Maneno yako yalete umoja na kuunganisha watu. Ni vizuri maneno yalete nguvu kwa watu na siyo udhaifu wala chuki. Yaonyeshe wewe ni kiongozi.

19. Utapata ubora kwa wengine kama na wewe ukitoa ubora wako. Kuna vitu viwili hapa navyo ni;
Kutoa na kupokea hivyo kama ukitoa ubora utapokea ubora. Kama ukitoa kitu ambacho kipo na kiwango cha chini utapokea matokeo ya chini pia.

20. Hii ndio siri ya kushinda. Kama unataka kushinda basi wasaidie wengine kushinda.
Ili upate mafanikio unahitaji usaidie watu kutatua matatizo yao nawe utapata kile unachotaka. Unapotatua shida ya mtu ndio ishara ya kufanikiwa kwani watu watalipia huduma unayotoa.

Nakutakia kila La heri Katika haya uliojifunza leo.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: