Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hili Ndilo Jambo Muhimu Ambalo Unaweza Kulifanya Hata Wewe Kwenye Maisha Yako

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu uko salama na unaendelea vizuri kuitendea haki zawadi ya siku hii ya leo. Chagua leo kuwa hii ni siku yako ya ushindi. Chagua kuwa na furaha siku hii ya leo na ishi katika mtazamo chanya siku zote. Karibu rafiki katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja.

Image result for no one limit you to do
Katika makala yetu ya leo tutajifunza somo linaloitwa hakuna aliyekukataza hata wewe unaweza kufanya. Karibu ndugu msomaji tuanze pamoja na tumalize pamoja katika safari yetu. Katika dunia ya sasa hakuna chumba au nafasi kwa walalamikaji yaani kuna watu wao kazi yao ni kuongea tu na kulalamika juu ya mambo yanayowatokea katika jamii zao bila kuchukua hatua yoyote.
Mpendwa rafiki,somo letu la leo linatualika kuwa hakuna anayekukataza hata wewe unaweza kufanya chochote katika maisha yako. Kuna maneno mengi ambayo watu utawasikia wakiongea kwa mfano, Fulani anafanya biashara Fulani aisee! Anapata kweli hela, au utasikia kitu Fulani kinalipa kweli huoni Fulani anavyoingiza na maisha yake yamebadilika? Swali la kujiuliza kama Fulani anafanya kitu na kinamsaidia kwani wewe umekatazwa kufanya?

soma;    Hiki Ndio Kitu Rahisi Sana Kukwepa Katika Maisha Yako Lakini Ni Ngumu Kukwepa Matokeo Yake
Hakuna mtu aliyekatazwa kufanya baishara,kilimo,kuandika ni wewe tu mwenyewe kuamua ufanye nini. Sasa muda wa kuongelea wenzako wanafanya kitu Fulani unao na hujapewa ruhusa na mtu sasa je unasubiri upewe ruhusa ili uanze kufanya ya kwako? Badala ya kuwaongelea wengine namna wanavyopiga hatua kimaendeleo na wewe unabidi uamke na uende ukafanye kwani hakuna aliyekukataza kufanya hata wewe unaweza.

 
Habari njema ni kwamba hakuna kizuizi cha umri katika mafanikio kwa mfano wewe ni kijana unajiona ni mdogo mno hivyo hustahili hakuna kitu kama hicho. Labda wewe ni mzee umri umeenda sana unaona hustahili lakini hakuna kitu kama hicho bado unaweza kufanya. Hakuna aliyekukataza kufanya jambo lolote la maendeleo la kupiga hatua katika maisha yako. Kibali cha kuanza unacho mwenyewe wala siyo mtu mwingine. Acha kuwaongelea wengine wanafanya mambo Fulani badala yake na wewe anza kufanya kwani hakuna aliyekukataza kufanya hata wewe unaweza.

SOMA HII;  Mambo Ishirini (20) Niliyojifunza Katika Kitabu Cha A Notes From A Friend
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: