Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Ishirini (20) Niliyojifunza Katika Kitabu Cha A Notes From A Friend

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? natumaini hujambo na unaendelea vizuri. karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza uchambuzi wa kitabu cha A notes from a friend kilichoandikwa na mwandishi Anthony Robbins. karibu rafiki nikushirikishe mambo niliyojifunza kupitia kitabu hiki.

Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha A Notes From A Friend na Anthony Robbins ni kama ifuatavyo ;
Karibu tujifunze kwa pamoja.

1. Tendo la ukarimu katika maisha ya binadamu ni tunda la unyenyekevu.
Ukarimu huwa unaponya kwenye kila sekta ya maisha yetu.
Mfano,mganga akimhudumia mgonjwa kwa ukarimu hata kama alikua anaumwa sana atapata nafuu kulingana na huduma unayompa kwa ukarimu.
Hivyo,maisha ni ukarimu tuitumie falsafa hii ya ukarimu kwenye maisha yetu ili kuifanya dunia kua sehemu salama ya kuishi.

2. Kuwa na fikra chanya peke yake haitoshi.
Kuwa na fikra chanya inahitaji matendo.
Tunahitaji kufanya vitu tofauti na tulivyozoea.
Kama ulikuwa mvuta sigara acha,kama ulikua mlevi acha ulevi na kama ulikua ni mtu unayehairisha mambo unatakia kuacha.
Haitoshi kuwa msomaji tu wa vitabu bali matendo.
Mtu akikuona mtaani ajue kabisa huyu ni mtu tofauti.

3. Kama ukibadilika wewe na watu watabadilika.
Unatakiwa kuwa mtu sahihi ili upate mtu sahihi.
Unatakiwa kua sehemu ya mabadiliko unayoyataka kuyaona duniani.
Ukianza mabadiliko utawakomboa wengi ,utaikomboa familia yako,utawakomboa marafiki wako nk.

4. Kile unachofanya sasa hivi ndio utambulisho wako katika safari yako.
Unatakiwa kuamini inawezekana. Mambo yaliyopita hayatakusaidia unatakiwa kuangalia mambo ya sasa.
Anza kubadili leo kwanza kwani leo ndio mwanzo wa safari.

5. Kuanzia leo unatakiwa kuondokana na dhana ya kwamba huwezi. Kila mtu anastahili kuweza.
Mtu ambaye anajitahilisha kua hawezi ni wewe mwenyewe. Ukijikubali na kujiamini unaweza utafika mbali.
Haijalishi jana ulifanya nini bali sasa unafanya nini.

6. Uvumilivu unalipa.
Siri ya mafanikio huwa ni uvumilivu.
Kitu muhimu katika maisha yako ni kugundua umuhimu wako nini na unatumiaje siku yako kwa vitendo kila siku kufanikisha malengo yako.
Hakuna aliyezaliwa anaweza bali kila kitu tunajifunza na katika kujifunza kila siku ni mchakato hivyo unatakiwa kua mvumilivu katika safari yako ya mafanikio.

7. Habari njema ni kwamba hakuna tatizo la kudumu katika maisha.
Hatakama leo umekwama na una matatizo ujue yataisha tu.
Usiache ndoto yako ipotee kwa sababu ya matatizo.
Unatakiwa kukomaa mpaka kieleweke.

8. Hakuna kufeli au kushindwa duniani.
Kama bado uko hai una nafasi ya kushinda pia na hutakiwi kukata tamaa.
Unaposhindwa katika jambo fulani huwezi kubaki hivyo hivyo kama ulivyokuwa mwanzo kwani utakua umejifunza kitu na kupata uzoefu ni wapi pa kuanzia mara ya pili tena.
Ukijaribu kufanya kitu na ukashindwa utakua umejifunza kitu.

9. Mafanikio ni matokeo ya hukumu nzuri.
Hukumu nzuri ni matokeo ya uzoefu.
Uzoefu ni mara nyingi huwa ni matokeo ya hukumu mbaya.
Tunajifunza kupitia makosa yetu. Hivyo basi, jibidiishe katika vitendo.

10. Tunapaswa kutambua kuwa ili tupate matokeo mapya tunapaswa kufanya matendo mapya kwanza.
Lakini matendo yetu yametawaliwa na maamuzi.
Nguvu ya maamuzi ni nguvu ya mabadiliko.
Hatuwezi kuzuia matokeo ya maisha yetu.
Lakini tunauwezo wa kuzuia nini tunataka kufikiri.
Kila mtu ni ana nguvu ya kuchagua.

11. Jinsi unavyoishi leo ni maamuzi uliyoyafanya.
Kama tukitaka kubadilisha maisha yetu tunatakiwa ya leo na kwenda kule tunapotaka kwenda tunatakiwa kufanya kitu kimoja nacho ni kufanya maamuzi mapya na matendo mapya.
Maamuzi ndio maisha.

12. Fomula ya ufunguo wa mafanikio ni kuamua kile unachotaka kwanza na mengine yatafuata.
Usikate tamaa hata kama umekataliwa ndoto yako mara ngapi haijalishi.
Uvumilivu wako na uthubutu wako ndio utakusaidia kukufikisha pale unapotaka kufika.
Usiseme hakuna njia bali sema kuna njia.

13. Njia pekee ya kubadilisha maisha yako ni kufanya maamuzi halisi.
Maamuzi halisi ni kuamini katika uwezekano.
Lenga katika kitu unachotaka. Kwa mfano, unataka kuacha kuvuta sigara lenga kuacha kuvuta sigara kwa vitendo na siyo natamani niache kuvuta sigara.
Maamuzi yako ndio yamebeba hatima ya maisha yako.
Amua leo kwa faida ya kesho.

14. Unatakiwa kujenga imani yako.
Nguvu ya msukumo inayosimamia maamuzi yako yote ni imani.
Imani yako ndiyo inakua kichocheo cha wewe kutenda jambo ambalo unaliamini.
Imani ni jicho lako la ndani ambalo linaona sehemu
ambayo wengine hawaoni.
Vitu vyote vimetawaliwa na imani yako kwani ndio nguvu iliyoshikilia maamuzi yako.

15. Mtakatifu Augustino aliwahi kusema, imani ni kuamini kile ambacho hujawahi kukiona kwa macho, na zawadi ya hii imani ni kuona kile ambacho unaamini.
Hivyo basi, unatakiwa kuamini kile unachofanya.
Unatakiwa kua na imani na kile unachofanya. Amini utafanikiwa kwanza hata kabla hujaanza kufanikiwa .
Imani uliyojiwekea katika akili yako ndio itakupa matokeo.
Amini na tenda ndio utaona matokeo kwa macho.

16. Kulenga kule unakotaka kwenda ndio kusudi la maisha.
Kwanza lengo lina linaweza kusaidia maisha yako.
Usikubali kutawaliwa na hofu badala yake unatakiwa kulenga kule unapotaka kwenda. Sasa kama huna lengo nayo ni tatizo njia yako inakua haina mwanga huko unapokwenda.
Unapolenga katika lengo lako mara nyingi utapata uzoefu.

17. Maswali ndio majibu ya njia yako. Njia bora ya kusimamia lengo lako ni kulenga katika kuuliza maswali yenye nguvu.
Unapouliza swali sahihi unaweza kuokoa/kusaidia maisha yako.
Injili ya mathayo sura ya 7 : 7 inasema ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtapata na bisheni nanyi mtafunguliwa.”
Usiache kuuliza pale unapotaka kupata jibu. Na usikose kubisha hodi pale unapotaka kufunguliwa.

18. Kila siku unatakiwa kujiuliza maswali.
Asubuhi unatakiwa kujiuliza maswali yenye nguvu.
Mfano wa maswali ni kama ; nini kinanifanya niwe na furaha sasa?
Nini ninachojivunia katika maisha yangu sasa . Ni jinsi gani unavyohisi ?
Nini kinakufanta uwe na shukurani?
Kuna maswali ambayo utajiuliza asubuhi na kuifanya akili iwe bora sana.
Hata jioni pia unatakiwa kujiuliza maswali kama vile umejifunza nini leo?
Nimetoa nini leo na nimekuwa mpokeaji au mtoaji?
Hivyo basi, maswali ni muhimu katika maisha yetu.

19. Unajisikiaje ukiwaona baadhi ya wenzako wameweza kufanikiwa na wewe bado huamini juu ya hili?
Jifunze kwa wenzako wakati sahihi ni sasa.
Ongea lugha yako na sikiliza muundo wa lugha za wengine. Na jifunze pia kutoka kwa wengine.
Hujazaliwa kushindwa bali umezaliwa kushinda.
Wewe ni mshindi wa maisha yako. Ongea lugha ya wanamafanikio.

20. Lengo la kua na malengo ni kupata muongozo au uelekeo wa kule unapotaka kwenda.
Mungu amempa kila mtu kipaji katika maisha miongoni mwa watu hao ni mimi na wewe.
Una uwezo mkubwa wa kufanya kile unachotaka kufanya. Unatakiwa kushindana na malengo yako na kufanya yale mambo ambayo watu wengi hawafanyi.
Weka malengo ambayo watu wengi hawayaweki katika maisha yako.
Nakutakia kila la heri na utekelezaji mzuri katika haya uliojifunza leo.
asante sana,
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: