Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndio Kitu Rahisi Sana Kukwepa Katika Maisha Yako Lakini Ni Ngumu Kukwepa Matokeo Yake

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini unaendelea vizuri na karibu tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja rafiki yangu. Unatakiwa kuchagua kuanza siku yako kila siku kwa furaha na hamasa kubwa hii ndio dalili ya kupata ushindi katika siku yako husika. Lakini ukichagua kuanza siku yako kwa huzuni yaani hali ya kutokuwa na furaha na hali ya kukata tamaa ujue unakwenda kuwa mshindwa na badala ya kuwa mshindi wa siku yako.

 
Mpendwa msomaji, katika makala yetu ya leo tutaweza kujifunza falsafa moja ya maisha ambayo inasema ukweli katika maisha yetu. Falsafa ni nzuri rafiki yangu kwani inakupa ukweli nao ukweli unakuweka huru. Sir Josiah aliwahi kusema hivi ‘’ it is easy to dodge our responsibility but it is difficult to dodge the consequences of our responsibility’’ akiwa na maana ya kwamba ni rahisi kukwepa majukumu au wajibu wetu lakini ni ngumu kukwepa matokeo ya wajibu wetu. Ni kweli kabisa huu ndio utamu wa falsafa unakupa uhalisia kabisa bila kuficha mambo.

 

Read more: http://www.amkamtanzania.com/2016/04/hizi-ndizo-faida-za-kufunga-ndoa-na.html#ixzz4MxexZJQN

Katika hali ya kawaida watu wengi wamekuwa ni watu wa kukwepa majukumu yao ya kila siku katika maisha lakini hawawezi kukwepa matokeo yake. Lazima itawagharimu tu. Kwa mfano, kijana mwenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea bado anakaa nyumbani anakwepa majukumu ya kujitegemea. Bado amekaa nyumbani akitegemea wazazi na kusubiri ukamilifu kwanza kumbe hajui ndio anapoteza muda na hawezi kukwepa matokeo yake. Jinsi unavyoanza mapema ndivyo unavyotengeneza mazingira mazuri ya kuwa bora zaidi baadae.

SOMA HAPA;Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yaoa-kukiandika-katika-maisha-yao

Tumelelewa katika jamii yetu na kuaminishwa kutojitegemea mapema na hii ndio athari mbaya sana kwa vijana wengi ambao matokeo yake hatuwezi kuyakwepa.
Jamii ya watu wa ulaya wanafurahia na kufanya sherehe pale mtu anapofikisha umri wa miaka kumi na nane (18) ambapo kisheria yuko huru katika maisha yake na kujitegemea. Kama wewe ni kijana unakwepa kujitegemea hakika huwezi kukwepa matokeo yake kama tulivyoona falsafa yetu ya leo ambayo inakuweka huru kabisa.

 
Kama unakwepa nakuoana ni hatari kuanza baishara sawa ni rahisi sana lakini ujue huwezi kukwepa matokeo yake. Kama unafanya kazi na huweki akiba yoyote wewe ni kula na kusubiria mwisho wa mwezi ni rahisi endelea kutumia lakini athari yake hutokuja kuikwepa. Kama unapata mshahara na unaishi juu ya kipato chako huwezi kukwepa matokeo yake. Kama unakwepa kunywa maji kila siku lakini huwezi kukwepa matokeo yake utaishiwa maji na utawekewa maji ya dripu.

 
Unakwepa kujenga mahusiano mazuri na familia yako, ndugu, jamaa na marafiki lakini kaa ukijua yakwapa huwezi kukwepa matokeo yake ya kukwepa kujenga mahusiano bora na wenzako. Unakwepa kumsamehe mwenzako na unaendelea kuvumilia lakini huwezi kukwepa uchungu unaendelea kuupata na kuishi maisha ya chuki ambayo hayana furaha. Umesahau kuwa kusamehe siyo kuvumilia? Ukiendelea kuvumilia unaendelea kubaki na uchungu moyoni ambao utakua unakusumbua na hutokuwa na raha katika maisha yako.

 
Tunakwepa kukua kiroho, kimwili na kiakili lakini matokeo yake hatuwezi kuyakwepa. Unawalea watoto katika malezi mabovu lakini huwezi kukwepa matokeo yake na wala jamii haiwezi kukwepa. Tumesahau ya kuwa ili tuwe na jamii bora tunapaswa kujenga familia bora. Msingi wa maisha ya binadamu yoyote unaanzia katika familia hivyo tukijenga familia bora na tutakuwa na jamii bora. Lakini tukikwepa kujenga misingi imara katika familia zetu hatuwezi kukwepa matokeo yake katika jamii zetu.

 
Hii sheria ya asili huwezi kuikimbia kabisa ukisema unakimbia changamoto katika maisha yako huwezi kukwepa matokeo yake hata kama umekaa ndani zitakufuata huko ulipo. Hapa duniani ni rahisi kukwepa majukumu yetu lakini ni ngumu kukwepa matokeo yake. Ukiwa unaishi maisha ya kuiga ni rahisi sana lakini matokeo yake huwezi kuyakwepa. Ni rahisi kuishi maisha ya kimazoea ambayo umeyakuta lakini huwezi kukwepa matokeo ya kuishi maisha ya kimazoea. Ni rahisi kukwepa mabadiliko lakini huwezi kukwepa matokeo yake ya kukwepa mabadiliko. Ni rahisi kuishi bila kuwa na muelekeo,malengo na mipango lakini ni ngumu kukwepa matokeo ya kuishi bila muelekeo.

 
Hivyo basi, ni rahisi kukwepa chochote katika maisha yako lakini ni ngumu kukwepa matokeo yoyote katika maisha yako. Tumia wakati wako vizuri na epuka kuahirisha mambo yako na ukikwepa kulipa gharama leo huwezi kukwepa matokeo yake.
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: